Saturday, August 13, 2016

udaku


Tuesday, March 29, 2016

image


Sunday, March 27, 2016

Serikali Yaanda Muongozo wa Ajira kwa Vijana


Kutokana na Tanzania kuwa na uchumi wa soko huria vijana wengi wameanza kushiriki katika sekta isiyo rasmi hivyo kunawafanya kuchangia nusu ya uchumi wa Taifa katika shughuli zao za kila siku.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel wakati akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza kuchukuliwa na serikali  ili kuhakikisha inawainua vijana kiuchumi.

Makble amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana na Serikali ili waweze kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha na kipato kizuri pamoja na mazingira mazuri ya kazi.

Mkurugenzi huyo amesema serikali imeanza kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia kwenye vipato vyao vya kila siku sambamba na kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.

Makbel ameongeza kuwa wahusika wakuu wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe mazingira rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa yakuchangia pato la taifa na serikali kuu wameanza vikao vya pamoja ili waone wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa vijana.

Saturday, March 26, 2016

Madereva Watatu wa Malori Wajeruhiwa Kwa Risasi na Mlinzi wa Hoteli


Madereva watatu wa malori yaendayo mikoani na wasaidizi wao watatu, wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwilini na mlinzi wa nyumba moja ya wageni iliyopo Ubena, Chalinze mkoani Pwani.

Tukio hilo limetokea jana alfajiri saa 11.30 kwenye hoteli hiyo ambako madereva na wasaidizi hao walikuwa wamefikia kwa mapumziko kabla ya kuendelea na safari. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventura Mushongi alisema tukio hilo lilitokea baada ya kuwapo kutokuelewana kati ya mmoja wa madereva na mlinzi wa nyumba hiyo.

Kamanda Mushongi alisema taarifa za awali zinasema baada ya mabishano hayo ambayo bado hayajajulikana chanzo chake, mlinzi huyo alikoki silaha yake aina ya Shortgun na kupiga risasi moja hewani kutuliza vurugu na kumjeruhi mmoja wa madereva hao.

Hata hivyo, mabishano yalizidi baada ya madereva wengine kujitokeza kuingilia ndipo mlinzi huyo akapiga risasi nyingine ambayo ilitoka na gololi zake kusambaa na kuwajeruhi wengine wanne ambao walipelekwa Kituo cha Afya Chalinze kwa matibabu.

Alisema mlinzi huyo amekimbia na anaendelea kutafutwa na chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Chalinze, Dk Victor Bamba alisema walipokea majeruhi watano ambao walipatiwa huduma ya kwanza na kutokana na hali zao kuwa mbaya walihamishiwa Hospitali ya Tumbi.

Akizungumza wodini Tumbi walikolazwa, mmoja wa madereva hao, Harun Adeli alisema walifika hapo juzi saa mbili usiku na kuamua kulala ndani ya magari yao ili jana waendelee na safari na ilipofika saa kumi na moja alfajiri walisikia makelele yanayoashiria ugomvi ndani ya hoteli hiyo.

“Wakati tunashangaa tulishtukia risasi zinarindima na ndipo zilipotufikia,” alisema.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Tumbi, Habibu Yahaya alisema aliwapokea majeruhi Stephen Fredy, Beno Henry, Akrey Dallu, Ramadhani Saidi, Amani Almasi na Adel wote wakazi wa Dar es Salaam.

Diwani wa Ubena, Nicolaus Muyunga alisema kwa mujibu wa majirani, yalitokea mabishano kati ya utingo na dereva ambao walikuwa wamekunywa na kulala kwenye meza muda mrefu, walipotakiwa kuchukua vyumba wakalale ndani au warudi katika magari yao walikataa na mlinzi alipotaka kuwaondoa kwa nguvu walimzidi nguvu, hivyo akajitetea kwa kupiga risasi hewani.

Mtoto wa Siku Moja Aibwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando


Mtoto wa siku moja ameibwa katika mazingira ya kutatanisha katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, akiwa pembeni mwa mama yake aliyekuwa amelala, mwenye umri wa miaka 16.

Akizungumzia uporaji huo jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha, amesema aliyepora mtoto huyo aliingia ndani ya wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando, akiwa amejifunga ushungi.

“Alipoingia wodini alikuta mama wa mtoto amesinzia akiwa peke yake wodini, ndipo akamuiba mtoto wake wa kike mwenye umri wa siku moja na kuondoka naye kwenda kusikojulikana,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kuhoji wauguzi, walinzi na wazazi waliokuwa wamelazwa wodini hapo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Kamugisha amesema Jeshi la Polisi mkoani humo, litaanza kufanya uhakiki wa silaha kuanzia Aprili mosi hadi Juni 30 mwaka huu, katika ofisi za makamanda wa Polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.

Amesema uhakiki wa silaha ni wa kitaifa na utahusu wamiliki binafsi, kampuni binafsi na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali zinazomiliki silaha.

“Lengo ni kupata kumbukumbu ya uhalali wa umiliki wa silaha. Watu wote wanaomiliki silaha watii agizo hili bila kulazimishwa, ili tufanikishe uhakiki kwa wakati na tuimarishe usalama katika mkoa wetu,” alisema.

Aliwataka watu wanaomiliki silaha isivyo halali, kusalimisha silaha hizo wenyewe kwenye ofisi za Serikali na kwa wakuu wa Polisi wa wilaya (OCD) kabla ya muda wa uhakiki wa silaha kumalizika.

“Baada ya hapo tutafanya msako kabambe wa watu waliokaidi kuhakiki silaha zao,” alisema.

KWELI DUNIA IMEISHA: GIGY MONEY ADAI YUPO TIYARI KUCHEZA PICHA CHAFU


Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

 Video Queen na msanii wa filamu Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameweka wazi kuwa yupo tayari kucheza picha za ngono endapo atapata mshiko wa maana.

Akistorisha na paparazi, Gigy alisema kwa kuwa anatafuta fedha ya kubadili maisha yake, anaweza kufanya tendo hilo kwa sababu anahitaji kuishi kitajiri zaidi kwani maisha ni matamu sana ila ni mafupi kwahiyo haoni sababu ya kutokujiachia.


Aliendelea kusema kuwa amewahi kufuatwa na watu mbalimbali kutoka Dubai wakimtaka kwenda kucheza filamu hizo, lakini alikataa kutokana na fedha walizomtajia kuwa ni kidogo na hakuwa tayari kwa muda huo ila kwasasa niko tiari, njooni tufanye business ila dau liongezeke.

“Yaani nikiambiwa napewa mamilioni nicheze picha hizo nipo tayari maana hapa duniani wanaokula starehe zaidi ni wale wenye fedha sasa nikipewa mamilioni ili nibadili maisha yangu, niko tayari maana nitabadili maisha yangu na nitaishi kitajiri hapo mpaka watu waje kunishtukia nitakuwa nimeshakula bata vya kutosha,” alisema Gigy. Hata hivyo Gigy hakutaja dau kamili la fedha anachohitaji ali acheze picha za ngono.

Gigy Money ni miongoni mwa ma-video Queen chipukizi wanaofanya vizuri katika video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

CHIDI BENZ APELEKWA BAGAMOYO SOBER HOUSE KWA AJILI KUMSAIDIWA KUACHA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA

Meneja wa Diamond, Babutale akishirikiana na Kalapina wamemchukua Chidi Benz na kumpeleka Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni rapa huyo kuomba msaada baada ya kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimkabili.
Kupitia instagram, Babutale amepost video na kuandika:
"Mwana amekubari kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini"
Katika video hiyo Babu Tale alisema wamefika salama Life and Hope Rehabilitation Organization, Huku Kalapina akiomba mungu kumsaidia Chidi Benz.

SIRI 5 NDOA YA WASTARA KUVUNJIKA!

WASTARA-X
WASTARA-X
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma siku ya harusi yake na mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma.



DAR ES SALAAM: Saa 24 tu tangu kupatikana kwa habari kwamba, ndoa ya staa wa sinema za Bongo, Wastara Juma aliyoifunga na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma imevunjika, sasa siri 5 za kuparaganyika kwa ndoa hiyo ziko mikononi mwa gazeti hili.

Ndoa hiyo ilidaiwa kuvunjika rasmi Machi 21, mwaka huu baada ya kuishi kwa siku 61 tangu kufungwa kwake, Januari 8, mwaka huu huko Tabata jijini Dar.


SIRI YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kimoja, miongoni mwa siri hizo zilizoisukuma ndoa hiyo kuvunjika ni kitendo cha Wastara kuomba kila kukicha kwamba, aachike baada ya madai kwamba, hakukuta furaha kama alivyotegemea.

“Wastara alitegemea kwamba baada ya kuolewa angekuta furaha. Lakini anavyosema jambo hilo silo alilokumbana nalo ndani ya ndoa. Hiyo ni siri moja wapo, ikamfanya Wastara amuombe Mungu kila siku ili aachike,” kilisema chanzo hicho.


wastara3563
….Akitabasamu siku ya harusi yake na mbunge huyo.

SIRI YA PILI
Chanzo kiliendelea kudai kuwa, pia Wastara aliingia kwenye ndoa hiyo huku moyo wake wote ukibaki kwa mchumba wake wa zamani, Bond Suleiman.

“Wastara tangu akiwa ndani ya maamuzi ya akubali au akatae kufunga ndoa na Sadifa, alikuwa akisema moyo wake umeelekea sana kwa Bond.

“Hivyo naamini kuwa, hata alipoambiwa anapewa talaka aliipokea kwa mikono miwili ili arudi kwa Bond. Mimi naamini hivyo,” kilisema chanzo.


WASTARA MWENYEWE NA SIRI NYINGINE
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wastara alikiri kuvunjika kwa ndoa yake huku akisema:
“Tangu nifunge ndoa sijawahi kuwa na furaha ndani ya ndoa hata mara moja kwani mume wangu alikuwa akinifanyia mambo siyo.


SIRI YA TATU
“Kabla hajanioa, aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunifungulia maduka kwa ajili ya kujiendeleza na vitu vingine vingi lakini hakuna hata kimoja alichokifanya,” alisema Wastara.


SIRI YA NNE
Staa huyo alikwenda mbele zaidi na kuanika siri ya nne akisema: “Nilipoona ndoa imenichosha nikawa najaribu kutishia kuondoka, nikimwambia naondoka alikuwa akiniambia njia nyeupe niondoke mapema ili mke wake (mkubwa) aje kuishi. Inaonekana alitamani niondoke ili mke wake aje kukaa nyumbani. Alisema mke wake hawezi kukaa hotelini na mimi nipo ndani.”

WASTARA4
….Akiwa na mashosti zake.


SIRI YA TANO
Ilidaiwa kuwa, siri nyingine iliyomfanya Wastara aachike ni kushindwa kwake kukabiliana na uke wenza hasa ikielezwa kuwa, uvumilivu wa hali ya juu unahitajika unapoingia kwenye ndoa ya sampuli hiyo.

“Unajua siri nyingine ni kwamba, Wastara siyo mwanamke wa kuvumilia uke wenzake, yapo baadhi ya mambo angevumilia lakini hakuwa mvumilivu, ikawa sababu ya yeye kuondoka,” alisema rafiki wa karibu wa staa huyo.


AONDOKA NA MSICHANA WA KAZI
Wastara alisema kuwa, ameamua kuondoka kwa mwanaume huyo yeye na msichana wake wa kazi ‘hausigeli’ kwa kuwa alishachoka.


ANACHOJUA WASTARA
“Mimi najua watu wengi watasema na kuniona tofauti lakini kikubwa naangalia furaha yangu iko sehemu gani, najuta sana kuingia kwenye ndoa lakini nawashauri wanawake wenzangu kufikiria mara mbilimbili kabla kuingia huko, kuna mambo mengi sana,” alisema Wastara.


HUYU HAPA MUME WA WASTARA
Sadifa Juma ndiye anayelalamikiwa na Wastara kwamba hakumtimizia yale aliyomwambia lakini pia ndiye anayedaiwa kumpa talaka Wastara na si kwamba, ameomba yeye.


WASTARA13
Akijibu madai ya Wastara alipoongea na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alisema:
“Mimi si mgonjwa wa akili, Wastara  ni mlemavu, hana baba wala mama halafu leo hii nimseme vibaya. Mpaka nimeamua kumuoa ina maana nilimpenda kwa nini nimfanyie vitu ambavyo sivyo?

“Lakini katika hayo, pia mimi nimefundwa kwa kufundishwa kwamba mambo ya ndoa hayapelekwi kwenye vyombo vya habari au Instagram. Na huyo aliyevianika vitu vya mke wangu nitadili naye.”


MSISITIZO WAKE
“Ninachojua mimi, Wastara bado ni mke wangu. Huyo mnayesema kwamba babu yake ameongea kwenye redio akisema kwamba nimemwacha Wastara, talaka alitoa yeye? Mambo ambayo mimi naweza kuyasema kwenye vyombo vya habari ni kuhusu jimbo langu au mambo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama changu.”


BOND: MIMI NIMESIKIASIKIA TU
Ijumaa lilimpigia simu Bond juzi na kumuuliza kuhusu Wastara kuachika ambapo alisema: “Na mimi nimesikiasikia na kusoma kwenye mitandao, hivi ni kweli?” (Ijumaa likaachana naye bila kumpa jibu).


MAISHA YA UHUSIANO, NDOA YA WASTARA
Wastara amapitia katika maisha ya uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa. Mwaka 2000 alifunga ndoa na mwanaume anayeitwa Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares.

Nyuma ya hapo, Wastara alizaa mtoto mmoja na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.

Mwaka 2003, Wastara alifunga ndoa na msanii mwenzake wa filamu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alifariki dunia mwaka, 2013. Walibahatika kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Farheen.


Mwaka 2015, akafunga ndoa na Mbunge Sadifa akitokea kwenye uhusiano na msanii wa filamu, Bond na aliyodai kuyasema ndiyo hayo kwamba ameachika kwa talaka mbili huku mumewe huyo akikanusha.

Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, habari zilitua Ijumaa kwamba Wastara ameugua ghafla baada ya sukari kupanda akiwa mjini Morogoro na kulazwa Hospitali ya ST. Herry Health


CREDIT:GPL

Sakata la Tumbili 61 Waliokamatwa Uwanja wa Ndege Lachukua sura Mpya


Serikali imeunda kikosi kazi kinachohusisha taasisi nyeti nchini kuchunguza sakata la kukamatwa kwa raia wawili wa Uholanzi wakiwa katika harakati za kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Kikosi hicho kinaundwa na maofisa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Kikosi cha Kupambana na Ujangili.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa aliwathibitishia wanahabari jana kuundwa kwa kikosi kazi hicho na kwamba, upelelezi wa sakata hilo umepamba moto.

“Upelelezi ndiyo kwanza bado mbichi, kwa hiyo siwezi kusema lolote kama lini watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa sababu upelelezi uko chini ya kikosi kazi hicho,” alisema Mutafungwa.

Juzi saa tano asubuhi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alitembelea Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kushuhudia wanyama hao.

Profesa Maghembe alisema kama kila kitu kitakwenda vizuri katika upelelezi, watuhumiwa wa kosa hilo watafikishwa mahakamani siku ya Jumanne.

Wanyama hao walikamatwa usiku wa kuamkia juzi katika uwanja huo wakati raia hao, Artem Alik Vardanyian (52) na Eduard Alik Vardanyian (44) wakiwa katika harakati za kuwasafirisha kwa kutumia ndege kubwa ya mizigo.

Hata hivyo, raia hao wa Uholanzi walikuwa na vibali vilivyotolewa na Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Charles Mulokozi ambaye tayari amesimamishwa kazi kwa kashfa hiyo.

Wanajeshi 8 wa JWTZ Watiwa Mbaroni Wakituhumiwa Kumuua Raia Waliyedai Kawaibia Simu Yao


Askari nane wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kigona wakituhumiwa kwa mauaji ya Erick Nilamewa (16) waliyemtuhumu kuwaibia simu moja aina ya Techno na Sh. 6,000.

Tukio hilo lilitokea juzi jioni Mtaa wa Mabatini Mwanga Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Wanajeshi hao wakiwa nane, walionekana wakimpiga Nilamewa kwa mateke, fimbo na kumchoma na pasi tumboni, kifuani na mgongoni, baada ya kumkamata wakimtuhumu kwa wizi huo.

Mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa Maweni.

Aidha, Ahamad Mussa, mkazi wa Mabatini eneo la Mwanga Manispaa ya Kigoma/Ujiji, amelazwa wodi namba 7 katika hospitali ya Mkoa Maweni kwa matibabu, kutokana na purukushani hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinard Mtui, alithibitisha kukamatwa kwa askari hao nane wa JWTZ  kwa tuhuma za mauaji ya  kijana huyo na kumjeruhi Mussa (16).

Mtui alisema “Ni kweli tunawashikilia wanajeshi nane na tunaendelea na upelelezi, na baada ya uchunguzi tutawapeleka mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.”

Akizungumza  kutoka kitandani alikolazwa, Mussa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kitwe, alitumiwa ujumbe wa simu na wanajeshi hao akiwa shuleni ambao walisema kwamba wanamhitaji.

“Baada ya kutumiwa ujumbe huo mimi nilimbipu, akanipigia na kujitambulisha kuwa yeye ni afande Aberi, akasema njoo mara moja nakuhitaji," alisema Mussa.

"Kwa sababu tunakaa mtaa mmoja, pia huwa naingiaga kwenye makazi yao wanaponituma vitu mbalimbali kama sigara, sikuwa na wasiwasi wowote kuhusu wito huo.”

Alisema alipofika alibisha hodi na walimwitikia na kumwambia akae uani ndipo baada ya muda alitoka Aberi akiwa amevaa kaptura ambaye alianza kuita wenzake ambao walianza kumsulubu.

“Nilimsikia akiwaita wenzake wakina afande Mayowa, Ally na wengine nimesahau majina yao lakini jumla walikuwa wanajeshi nane ambao walikuwa wakinipiga.

"Waliniambia ninyooshe miguu yangu juu ya ukuta na niliponyoosha walinipiga na ubao na fimbo ya mianzi kichwani… damu zilianza kutoka.

"Wakachukua maji wakasafisha, wakapiga tena kichwa nikaanguka chini kisha wakanipiga mateke na kunichapa na nyaya za umeme huku wakiuliza ilipo simu na Sh 6,000 nilizoiba,” alisema Mussa.

Alisema wakati hali ikizidi kuwa mbaya, "walichukua chupa ya pombe na kunimiminia" kabla ya kujitokeza mwanamke mmoja wa nyumba ya jirani anayefahamika kwa jina la mama Hoza ambaye aliwaambia wamwache "mtoto wa watu maana watamuua bure.
 
“Mimi sijaiba simu wala siku ya leo (jana) sijafika kambini hapo.

"Sijaiba wao wakaendelea kunipiga na kunimwagia maji na kunigalagaza kwenye mchanga wakati huo damu zinaendelea kuvuja kichwani, ndipo mimi nikawambia naomba niende nyumbani nikamwambie mama yangu na tulienda na mwanajeshi mmoja na tulipofika nyumbani tulimkuta mama yangu.

"Mwanajeshi huyo akasimama nje mimi nikaingia ndani nikapita uani na kukimbia na ndiyo ikawa pona yangu la sivyo na mimi ningefariki dunia.”

Alisema baada ya yeye kukimbilia ndipo walipomkamata Erick mtaani na kumpeleka kwenye makazi yao ambako walimpiga na kumtesa hadi walipoona hali yake kuwa mbaya, walikwenda polisi kuchukua fomu namba 3 (PF3)kwa ajili ya kumpeleka hospitali ya Maweni kwa matibabu, lakini alifariki dunia.

Mama mzazi wa majeruhi huyo, Mwaisala Ahamad (36) alisema wanajeshi walimuagiza mtoto mmoja kwenda nyumbani kwake kwamba wanamuitaji mtoto wake na aliwaambia kuwa ameende shuleni.

“Waliniomba namba ya simu ya mtoto wangu nikawapatia kwasabababu wanajeshi hawa walikuwa na mazoea na mwanangu,"alisema Mwaisala.

"Nilipowapa nilienda kwenye shughuli zangu kama kawaida sikuwa na wasiwasi wowote, hawa tunawajua.

"Wengine wana nyota moja (luteni nusu) na wengine mbili (luteni) na wengine tatu (kepteni) na kutokana na vyeo walivyokuwa navyo sikutarajia mtoto wangu yamkute yaliyomkuta.”

Aliongeza kuwa kama askari hao walihisi kuwa mtoto wake ndiye aliyeiba simu yao walipaswa kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mshumbusi Edmond alithibitisha kumpokea marehemu Nilamewa akiwa na majerahe kifuani, tumboni na mgongo lakini akafariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Mwili wake uko chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa Maweni, alisema.

Waliokula mishahara HEWA Singida kusherehekea siku ya Wajinga Rumande


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe ameagiza mamlaka zinazohusika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu watakaobainika kutafuna fedha za mishahara hewa kabla ya mwezi huu kumalizika.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha kufahamiana kilichohudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa idara ya sekretarieti ya mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ofisini kwake.

Katika hotuba yake fupi na ambayo haikuwa na mbwembwe za kisiasa, alisema uhakiki uliofanyika hivi karibuni mkoani humo ulibainika kuwa na wafanyakazi hewa wengi, jambo linaloonyesha kuwapo kwa ubadhirifu wa kiwango cha juu cha fedha za umma.

“Naagiza kila mmoja wenu akaangalie kwenye taasisi yake iwapo wafanyakazi wanaolipwa mishahara ndiyo hao waliopo kazini au la. Kuna madai wastaafu, waliohama na hata watumishi waliokufa mishahara yao bado inalipwa hadi hivi leo,”alisema.

“Iwapo itagundulika kuwa kuna watu walioshiriki katika ulaji huo wa fedha za umma, wakamatwe mara moja ifikapo Aprili Mosi, mwaka huu na kufikishwa kunakohusika haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.”

Mtigumwe aliwakumbusha viongozi hao umuhimu wa watumishi walio chini yao kufanya kazi kwa uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

“Haiwezekani mtu atoke kijijini kisha arudi bila kuhudumiwa, lazima kuwahi kazini na kukaa hadi mwisho wa saa za kazi,” alisema.

Pia, alisisitiza umuhimu wa kila taasisi ya Serikali mkoani humo kufungua kitabu cha kero za wananchi na kuhakikisha zinaorodheshwa na kuonyesha hatua halisi iliyofikiwa katika kuzishughulikia.
 

JIJI LETU Copyright © 2011 -- Template created by O Pregador -- Powered by Blogger