Tuesday, May 23, 2017

img4


image3


Sunday, May 14, 2017

image2


image1


Monday, May 8, 2017

Sportpesa yahamia kwa Simba na Yanga

THAMANI ya Ligi Kuu ya Kenya maarufu kama Kenya Premier League imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa na kuanza kurejesha heshima ya soka la Kenya.

Kabla, soka la Kenya lilionekana limepoteza mvuto kabisa na kwa zaidi ya misimu nane limekuwa likisuasua na kuandamwa na migogoro ya kila aina.

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), chini ya mkongwe Sam Nyamweya lilionekana kupoteza mwelekeo na mambo yakazidi kuwa magumu.

Ilifikia wakati kukawa na ligi mbili ndani ya nchi moja. Ligi moja ilisimamiwa na FKF na nyingine bodi ya ligi.

Mwisho wa msimu, kukawa na bingwa wawili, washindi wa pili wawili halikadhalika watatu na wengineo. Hii ilikuwa ni sehemu ya kuonyesha kwamba soka la Kenya limekosa mwelekeo kabisa.

Miaka minne iliyopita wakati Nyamweya anakaribia kuondoka, timu ya taifa ya Kenya “Harambee Stars” chini ya Kocha Adel Amrouche, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji lililofanyika nchini humo.

Wengi walishangazwa na sifa nyingi zikaenda kwa kocha Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria. Kwamba ana uwezo wa kufanya katika mazingira magumu kama alivyokuwa akiifundisha Burundi.

Uchaguzi uliofuata, Nyamweya aliangushwa na Nick Mwendwa, akiwa ni rais kijana kushika nafasi hiyo. Wengi waliingiwa hofu angeweza vipi kuendesha mambo naye alikubaliana na hali haikuwa nzuri.

Mwaka wa kwanza, hali ilionekana kuzidi kuwa ngumu na ule usemi kwamba angekwama ukazidi kuchukua nafasi.
Lakini wakati ikionekana na Mwendwa alikuwa ameshindwa, ghafla mambo yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi kubwa.

Wengi wakaonekana kushangazwa kwa kuwa Kenya ilikuwa kati ya timu zilizokuwa chini ya kiwango cha 130 katika viwango vya soka vya Fifa. Hawakuwa tena na tofauti na Tanzania ambao angalau walikuwa na nafuu.

Utaona ule mlolongo wa wachezaji wengi wa Kenya na hata Uganda kukimbilia Tanzania ulizidi kuongezeka kwa kuwa hata zile timu kama Sofapaka zilizokuwa zikilipa vizuri zilidorora na wakongwe Gor Mahia na AFC Leopards walikuwa wameyumba na kuonekana hawana nafasi kwani kila walipoinuka walianza kuyumba tena.

Mwendwa akaonekana ni shujaa, lakini ukweli ni udhamini mnono ambao walianza kuufanya kampuni ya masuala ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.

SportPesa walidhamini timu zote kongwe mbili za Gor Mahia na AFC Leopard na kawaida wao ndiyo chachu ya ushindani. Pia wakadhamini timu nyingine na Nakuru All Stars.
Kama hiyo haitoshi, kampuni hiyo ikaingiza udhamini mnono katika Ligi Kuu Kenya na kufanya kuwe na ushindani zaidi kwa kuwa fedha hizo zinaingia kwenye mifuko ya timu zote 18 zinazoshiriki ligi hiyo.

Ukiangalia thamani ya ligi ya Kenya imepanda, ushindani umerudi na hamasa hata ya mashabiki kwenda viwanjani imerudi kwa kasi kubwa na sasa ni kati ya ligi zilizo juu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Taarifa zimekuwa zikieleza SportPesa tayari wako nchini na wamenuia kuzidhamini Yanga na Simba ambazo ni timu zenye mashabiki zaidi katika ukanda huu.

Inawezekana siku moja wakaingia kwenye ligi lakini kampuni hiyo kama itatumika vizuri basi inaweza kurejesha hamasa tena.

Huenda tuaona kawaida lakini mfano mzuri, Simba kwa msimu mzima wa 2016-17 imecheza kwa hasara kama tulivyowahi kuandika makala.

Kwamba hawana mdhamini na vifua vyao ni mali, lakini hakukuwa na aliyeona thamani yao baada ya kujiondoa kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Shukrani kwa TBL kwa kuwa waliweza kujali angalau kwa misimu kadhaa. Lakini kama SportPesa basi ndiyo wakati mwingine wa kurejesha heshima ya soka nchini.

Hakuna unapoweza kukwepa fedha katika maendeleo ya soka. Vizuri pia kufanya kazi na watu waliojifunza kupitia hatua mbalimbali.

Mfano SportPesa wanadhamini timu ya Ligi Kuu England (EPL), Hull City. Unapozungumzia udhamini wanajua nini cha kufanya kusaidia zaidi.

Kawaida wadhamini walioendelea hupenda mafanikio kwa wale wanaowadhamini. Hii ni nafasi kwa Yanga na Simba kubadili mambo na hasa kama wataingia udhamini, basi fedha watakazozipata ziwe kwa ajili ya maendeleo na si mifuko ya wahusika.

SportPesa ni sehemu wa wadhamini wa klabu maarufu ya Arsenal ya England. Hivyo wanajua kitu kinachoweza kuwasaidia Yanga na Simba lakini soka la Tanzania.

Kikubwa ambacho SportPesa wamekuwa wakikifanya ni kurudisha kiasi cha fedha kwa jamii kama udhamini. Wameweza kuzirudisha Gor Mahia na AFC Leopards katika ramani ya soka zikiwa na nguvu.

Simba na Yanga hazikuwa zimekufa lakini mwendo wao ulikuwa unaashiria “kifo”. Sasa ndiyo wakati mwafaka wa kutumia vizuri udhamini huo unaelezwa kuwa utakuwa mkubwa zaidi kuliko waliowahi kupata hapo awali.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaifutia leseni benki ya FBME

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeifutia leseni ya biashara Benki ya FBME na kuteua Bodi ya Bima ya Amana  kuwa mfilisi kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa na BoT inawataka wenye amana, wadai na wadaiwa kuwa wavumilivu wakati mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.

“Mfilisi kwa wakati muafaka atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa  utaratibu wa malipo ya madai, ulipaji wa madeni  na taratibu nyingine zinazohitajika kwa mujibu wa sheria,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Uamuzi huu wa BoT umetolewa baada ya hukumu ya kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikiikabili benki hiyo kutolewa.

Itakumbukwa, mwaka 2014, Mtandao wa Kudhibiti Uhalifu wa Masuala ya Fedha (FinCEN) wa Marekani uliitaja FBME kuwa taasisi inayojihusisha na utakatishaji fedha hivyo kuizuia kutoa huduma nchini humo.

Machi mwaka jana, msimamo wa FinCEN uliendelea kuwa huohuo hata Aprili 14, mahakama moja jijini Washington, DC ilitoa hukumu inayoupendelea mtandao huo. Nakala za hukumu hiyo imetumwa kwa BoT na Benki Kuu ya Cuprus kwa hatua zaidi.

Baada ya hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Christopher Cooper, benki hiyo yenye makao makuu yake nchini na matawi huko Cyprus italazimika kurudisha Dola 2.6 bilioni za Marekani ambazo ni amana za wateja wake ndani ya siku 90.


MUHIMU:Hivi Ndiyo Earphone Zilivyo Hatari Kwenye Masikio


Kundi kubwa la watu watumiaji wa spika ndogo za masikioni (earphone), hasa wanahabari na wanafunzi, wako hatarini kupata magonjwa mbalimbali yanayotokana na vijidudu vinavyoambukiza, uchunguzi umebaini.
Uchunguzi huo umebaini kuwa ni jambo lililozoeleka kwa wanahabari wanapokuwa vyumba vya habari au maofisini, kuazimana spika hizo bila kuchukua tahadhari za kiafya.
Mbali na kundi hilo, kundi kubwa la vijana wadogo, hasa wanafunzi, pia liko katika hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya masikio kutokana na mazoea hayo ya kuchangia matumizi ya spika hizo.


Watu mbalimbali waliohojiwa, wameelezea kutoelewa athari zinazoweza kusabishwa na kuchangia earphone ambazo huweza kubeba magonjwa ya ngozi na yale ya masikio kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Dk Kareem Segumba alisema uchangiaji wa ‘earphone’ si jambo zuri kwa kuwa husababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutoka kwa mtu mmoja aliyeathirika kwenda kwa mwingine.
“Kitaalamu tunasema anapata contagious (maambukizi) ya magonjwa ya sikio toka kwa mgonjwa. Magonjwa haya ni pamoja na fungus ya masikio,” alisema Dk Kareem.
Dk Kareem, ambaye amehudumu katika hospitali mbalimbali nchini, alitaja magonjwa mengine kuwa ni maambukizi ya sikio sehemu ya mzunguko na maambukizi kwenye ngoma ya sikio.


“Mara nyingi mtu anayeumwa fangasi ya sikio au kutokwa na majimaji kidogo kabla ya kugeuka usaha huwa hawajitambui. Wengi wanajua baada ya kuona usaha,” alisema.
“Si desturi nzuri kuchangia earphone na mtu yeyote kwa kuwa madhara yake ni makubwa na hasa ukizingatia masikio yako karibu sana na ubongo na huenda ukapata maambukizi kupitia mishipa.
“Mishipa ya damu inapeleka vijidudu vya ugonjwa kwenye ubongo na hatimaye kutokea athari nyingine kama uziwi, kupoteza nguvu ya kuona na matatizo kwenye uti wa mgongo.”
Mpigapicha wa kituo cha televisheni cha ITV mkoani Kilimanjaro, Robert Minja alikiri watu wengi hususan wanahabari wamekuwa na tabia ya kuchangia earphone, kwa vile hawajui madhara.


“Hilo la ku- share earphone (kuchangia) lipo sana na inavyoonekana watu wengi hawajui madhara yake. Tunaona ni mambo ya kawaida lakini kiukweli hii tabia ina madhara ya kiafya,” alisema.
Maulid Rashid, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (Smmuco) alisema tatizo la kuchangia vifaa hivyo ni kubwa chuoni hapo.
“Ni kweli wanafunzi wengi wanachangia hizo earphone. Nafikiri wanaofanya hivyo hawana uelewa kuwa kuna madhara. Yaani hili ni tatizo kubwa si kwa wanafunzi tu hata watu wa kawaida,” alisema.


Saturday, August 13, 2016

udaku


Tuesday, March 29, 2016

image


Sunday, March 27, 2016

Serikali Yaanda Muongozo wa Ajira kwa Vijana


Kutokana na Tanzania kuwa na uchumi wa soko huria vijana wengi wameanza kushiriki katika sekta isiyo rasmi hivyo kunawafanya kuchangia nusu ya uchumi wa Taifa katika shughuli zao za kila siku.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel wakati akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza kuchukuliwa na serikali  ili kuhakikisha inawainua vijana kiuchumi.

Makble amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana na Serikali ili waweze kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha na kipato kizuri pamoja na mazingira mazuri ya kazi.

Mkurugenzi huyo amesema serikali imeanza kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia kwenye vipato vyao vya kila siku sambamba na kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.

Makbel ameongeza kuwa wahusika wakuu wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe mazingira rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa yakuchangia pato la taifa na serikali kuu wameanza vikao vya pamoja ili waone wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa vijana.
 

JIJI LETU Copyright © 2011 -- Template created by O Pregador -- Powered by Blogger