![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIC8lKgruOHfxf9NnVQ3hvGV8CVMdXM3PsPbYFllyjVF3Xw5MW9b1aqRc4NdLlTnZHkw7ReGbu3AdnmqSSHh7lKP_ZKpgo3nVCPJRmasGTDl-c_f8O75NKIebivmXRhL38FVu-OHT35GvR/s640/1.jpg)
Benki
Kuu ya Tanzania (BoT) imeifutia leseni ya biashara Benki ya FBME na
kuteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa mfilisi kuanzia leo.
Taarifa
iliyotolewa na BoT inawataka wenye amana, wadai na wadaiwa kuwa
wavumilivu wakati mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki
zao.
“Mfilisi
kwa wakati muafaka atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa
utaratibu wa malipo ya madai, ulipaji wa madeni na taratibu nyingine
zinazohitajika kwa mujibu wa sheria,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Uamuzi huu wa BoT umetolewa baada ya hukumu ya kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikiikabili benki hiyo kutolewa.
Itakumbukwa,
mwaka 2014, Mtandao wa Kudhibiti Uhalifu wa Masuala ya Fedha (FinCEN)
wa Marekani uliitaja FBME kuwa taasisi inayojihusisha na utakatishaji
fedha hivyo kuizuia kutoa huduma nchini humo.
Machi
mwaka jana, msimamo wa FinCEN uliendelea kuwa huohuo hata Aprili 14,
mahakama moja jijini Washington, DC ilitoa hukumu inayoupendelea mtandao
huo. Nakala za hukumu hiyo imetumwa kwa BoT na Benki Kuu ya Cuprus kwa
hatua zaidi.
Baada
ya hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Christopher Cooper, benki hiyo yenye
makao makuu yake nchini na matawi huko Cyprus italazimika kurudisha Dola
2.6 bilioni za Marekani ambazo ni amana za wateja wake ndani ya siku
90.