![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEidzMwus1Lzlze80nxBcXa65i3SqjAhB8MCHvfSdxbjyOdR_I19uVInOH_07AR0Kj8C-yFY66tHCr94-hXI_5l0pShsRI7t9MkJRIYinRsMbxG8hISWbcgwc71JyznGy9GVRk_SK-KD/s640/gor_thikawin.jpg)
THAMANI ya Ligi Kuu ya Kenya maarufu kama Kenya Premier League
imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa na kuanza kurejesha heshima ya soka la
Kenya.
Kabla, soka la Kenya lilionekana limepoteza mvuto kabisa na kwa zaidi ya misimu nane limekuwa likisuasua na kuandamwa na migogoro ya kila aina.
Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), chini ya mkongwe Sam Nyamweya lilionekana kupoteza mwelekeo na mambo yakazidi kuwa magumu.
Ilifikia wakati kukawa na ligi mbili ndani ya nchi moja. Ligi moja ilisimamiwa na FKF na nyingine bodi ya ligi.
Mwisho wa msimu, kukawa na bingwa wawili, washindi wa pili wawili halikadhalika watatu na wengineo. Hii ilikuwa ni sehemu ya kuonyesha kwamba soka la Kenya limekosa mwelekeo kabisa.
Kabla, soka la Kenya lilionekana limepoteza mvuto kabisa na kwa zaidi ya misimu nane limekuwa likisuasua na kuandamwa na migogoro ya kila aina.
Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), chini ya mkongwe Sam Nyamweya lilionekana kupoteza mwelekeo na mambo yakazidi kuwa magumu.
Ilifikia wakati kukawa na ligi mbili ndani ya nchi moja. Ligi moja ilisimamiwa na FKF na nyingine bodi ya ligi.
Mwisho wa msimu, kukawa na bingwa wawili, washindi wa pili wawili halikadhalika watatu na wengineo. Hii ilikuwa ni sehemu ya kuonyesha kwamba soka la Kenya limekosa mwelekeo kabisa.
Miaka minne iliyopita wakati Nyamweya anakaribia kuondoka, timu ya taifa
ya Kenya “Harambee Stars” chini ya Kocha Adel Amrouche, ilifanikiwa
kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji lililofanyika nchini humo.
Wengi walishangazwa na sifa nyingi zikaenda kwa kocha Amrouche raia wa
Ubelgiji mwenye asili ya Algeria. Kwamba ana uwezo wa kufanya katika
mazingira magumu kama alivyokuwa akiifundisha Burundi.
Uchaguzi uliofuata, Nyamweya aliangushwa na Nick Mwendwa, akiwa ni rais
kijana kushika nafasi hiyo. Wengi waliingiwa hofu angeweza vipi
kuendesha mambo naye alikubaliana na hali haikuwa nzuri.
Mwaka wa kwanza, hali ilionekana kuzidi kuwa ngumu na ule usemi kwamba angekwama ukazidi kuchukua nafasi.
Lakini wakati ikionekana na Mwendwa alikuwa ameshindwa, ghafla mambo yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi kubwa.
Wengi wakaonekana kushangazwa kwa kuwa Kenya ilikuwa kati ya timu
zilizokuwa chini ya kiwango cha 130 katika viwango vya soka vya Fifa.
Hawakuwa tena na tofauti na Tanzania ambao angalau walikuwa na nafuu.
Utaona ule mlolongo wa wachezaji wengi wa Kenya na hata Uganda
kukimbilia Tanzania ulizidi kuongezeka kwa kuwa hata zile timu kama
Sofapaka zilizokuwa zikilipa vizuri zilidorora na wakongwe Gor Mahia na
AFC Leopards walikuwa wameyumba na kuonekana hawana nafasi kwani kila
walipoinuka walianza kuyumba tena.
Mwendwa akaonekana ni shujaa, lakini ukweli ni udhamini mnono ambao
walianza kuufanya kampuni ya masuala ya michezo ya kubahatisha ya
SportPesa.
SportPesa walidhamini timu zote kongwe mbili za Gor Mahia na AFC Leopard
na kawaida wao ndiyo chachu ya ushindani. Pia wakadhamini timu nyingine
na Nakuru All Stars.
Kama hiyo haitoshi, kampuni hiyo ikaingiza udhamini mnono katika Ligi
Kuu Kenya na kufanya kuwe na ushindani zaidi kwa kuwa fedha hizo
zinaingia kwenye mifuko ya timu zote 18 zinazoshiriki ligi hiyo.
Ukiangalia thamani ya ligi ya Kenya imepanda, ushindani umerudi na
hamasa hata ya mashabiki kwenda viwanjani imerudi kwa kasi kubwa na sasa
ni kati ya ligi zilizo juu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Taarifa zimekuwa zikieleza SportPesa tayari wako nchini na wamenuia
kuzidhamini Yanga na Simba ambazo ni timu zenye mashabiki zaidi katika
ukanda huu.
Inawezekana siku moja wakaingia kwenye ligi lakini kampuni hiyo kama itatumika vizuri basi inaweza kurejesha hamasa tena.
Huenda tuaona kawaida lakini mfano mzuri, Simba kwa msimu mzima wa 2016-17 imecheza kwa hasara kama tulivyowahi kuandika makala.
Kwamba hawana mdhamini na vifua vyao ni mali, lakini hakukuwa na
aliyeona thamani yao baada ya kujiondoa kwa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL).
Shukrani kwa TBL kwa kuwa waliweza kujali angalau kwa misimu kadhaa.
Lakini kama SportPesa basi ndiyo wakati mwingine wa kurejesha heshima ya
soka nchini.
Hakuna unapoweza kukwepa fedha katika maendeleo ya soka. Vizuri pia kufanya kazi na watu waliojifunza kupitia hatua mbalimbali.
Mfano SportPesa wanadhamini timu ya Ligi Kuu England (EPL), Hull City.
Unapozungumzia udhamini wanajua nini cha kufanya kusaidia zaidi.
Kawaida wadhamini walioendelea hupenda mafanikio kwa wale
wanaowadhamini. Hii ni nafasi kwa Yanga na Simba kubadili mambo na hasa
kama wataingia udhamini, basi fedha watakazozipata ziwe kwa ajili ya
maendeleo na si mifuko ya wahusika.
SportPesa ni sehemu wa wadhamini wa klabu maarufu ya Arsenal ya England.
Hivyo wanajua kitu kinachoweza kuwasaidia Yanga na Simba lakini soka la
Tanzania.
Kikubwa ambacho SportPesa wamekuwa wakikifanya ni kurudisha kiasi cha
fedha kwa jamii kama udhamini. Wameweza kuzirudisha Gor Mahia na AFC
Leopards katika ramani ya soka zikiwa na nguvu.
Simba na Yanga hazikuwa zimekufa lakini mwendo wao ulikuwa unaashiria
“kifo”. Sasa ndiyo wakati mwafaka wa kutumia vizuri udhamini huo
unaelezwa kuwa utakuwa mkubwa zaidi kuliko waliowahi kupata hapo awali.